• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Rwanda yalenga kuwekeza dola milioni 90 sekta ya kilimo.

    (GMT+08:00) 2018-10-16 19:28:15

    Serikali ya Rwanda inalenga uwekezaji wa dola milioni 90 kwenye sekta ya kilimo.

    Halmashauri ya maendeleo na wizara ya kilimo nchini humo pia zinatafuta masoko ili kuongeza uuzji wan je na kufungua nafasi za ajira.

    Maafisa wa wizara na halmashauri hiyo wamesema hayo kwenye mkutano wa kilimo biashara ulioleta pamoja watunga sera na wadau wa kiilimo.

    Zaidi ya wawekezaji 200 wameshiriki mkutano huo chini ya maudhui ya kilimo na maendeleo ya kilimo biashara.

    Mkurungezi mkuu wa halamashauri ya maendeleo Clare Akamanzi, amesema kuwa sekta ya kibinafsi imeendelea kutekeleza wajibu muhimu kwenye kilimo na hivyo kusaidia ukuaji wa uchumi wa nchi.

    Sekta ya kilimo nchini Rwanda huchangia asilimi 30 ya pato la taifa na kuajiri asilimia 70 ya wakaazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako