• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na mwenyekiti wa Klabu ya Makundi 48 ya Uingereza

    (GMT+08:00) 2018-10-16 20:56:22

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na mwenyekiti wa Klabu ya Makundi 48 ya Uingereza inayoshughulikia kuhimiza mawasiliano ya biashara kati ya Uingereza na China Bw. Stephen Perry.

    Rais Xi amesema watu wa China wanafanya jitihada mfululizo kwa ajili ya kutimiza "malengo mawili ya mia moja". Amesema huu ni mwaka wa 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, na katika miaka hiyo, China imepata mafanikio makubwa. Ameongeza kuwa, China inatetea kujenga jumuiya binadamu yenye hatma ya pamoja, na kuendeleza urafiki kati ya nchi tofauti, na pia inajitahidi kujenga "zama ya dhahabu" ya uhusiano kati yake na Uingereza.

    Bw. Perry amesema Klabu ya Makundi 48 inajishughulisha na kuhimiza mawasiliano kati ya China na dunia, na kupenda kujiunga na mchakato wa ustawi wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako