Baraza la Katiba la Cameroon limekataa maombi 16 kati ya 18 yanayotaka kubatilisha baadhi au kura zote zilizopigwa katika uchaguzi mkuu wa tarehe 7, Oktoba nchini humo. Wanasheria wa Bw. Cabral Libbi, mgombea wa chama cha upinzani cha Univers, walitetea kuwa uchaguzi huo unapaswa kubatilishwa kwani haukufanyika kwa uhuru, haki wala uwazi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |