• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Kufuzu Afcon 2019: Tanzania yalipa kisasi kwa Cape Verde, Uganda nayo yashinda

  (GMT+08:00) 2018-10-17 09:19:45

  Mjini Dar es Salaam jana, timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Cape Verde katika mechi ya kufuzu Afcon 2019.

  Magoli ya Tanzania yalifungwa na Simon Msuva na Mbwana Samata, na kuifanya timu hiyo ishike nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi L kwa kufikisha alama 5.

  Uganda ambayo ilishinda mechi yake ya jana kwa magoli 2-0 dhidi ya Lesotho ndiyo inaongoza kundi L kwa kuwa na alama 10.

  Katika kundi hilo, kila timu imebakiza mechi mbili ili kukamilisha mzunguko wa kufuzu, na baada ya hapo timu ya kwanza na timu ya pili kwenye msimamo ndizo zitakazofuzu Afcon 2019.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako