• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uturuki inaweza kuwahoji maofisa wa Saudi Arabia kuhusiana na mwanahabari aliyepotea

    (GMT+08:00) 2018-10-17 09:26:31

    Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Bw. Mevlut Cavusoglu amesema kama kukiwa na haja, Uturuki inaweza kuwahoji maofisa wa Saudi Arabia kuhusiana na tukio la kupotea kwa mwanahabari wa Saudi Arabia Bw. Jamal Kashoggi.

    Bw. Cavusoglu amesema idara ya mwendesha mashtaka ya Uturuki, inaweza kuamua nani wa kumhoji kama wana maswali. Bw. Cavusoglu amesema hayo wakati Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo aliyekuwa ziarani nchini Saudi Arabia, anatarajia kufanya ziara nchini Uturuki, na amesema anatarajia kuwa Bw. Pompeo ataleta habari mpya.

    Wakati huo huo Umoja wa mataifa umesema unasubiri kupata taarifa za undani wa tukio la Bw. Kashoggi, kabla ya kutoa maoni yoyote kuhusu tukio hilo. Habari zinasema Bw. Kashoggi aliuawa na maofisa wa Saudi Arabia kwenye ofisi ya ubalozi wa nchi hiyo mjini Istanbul, na mwili wake ulikatwa vipande vipande na kusafirishwa nje ya nchi kwa fuko la kidiplomasia. Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman amesema hafahamu lolote kuhusu kupotea kwa mwanahabari huyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako