• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matumizi ya Internet barani Afrika yameongezeka mara tatu ndani ya miaka mitano

    (GMT+08:00) 2018-10-17 09:26:51

    Bara la Afrika limekuwa moja ya maeneo yenye viwango vikubwa vya maendeleo ya matumizi ya internet duniani, na katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ongezeko hilo limekuwa mara tatu.

    Kwenye mkutano wa kwanza wa Afrika kuhusu uhalifu wa mtandao wa internet barani Afrika, unaofanyika mjini Addis Ababa, kuanzia tarehe 16 hadi 18, Umoja wa Afrika umesema matumizi ya internet barani Afrika yameongezeka mara tatu ndani ya miaka mitano. Hata Umoja wa Afrika umeonya kuhusu ongezeko la tishio la usalama wa mtandao wa internet, kutokana na maendeleo ya Tehama, na kuwepo kwa huduma za hali ya juu na apps zake.

    Baadhi ya hatari zilizotajwa ni pamoja na hotuba za chuki, chuki dhidi ya wageni na ubaguzi wa rangi, vinavyochochea siasa kali na matumizi ya mabavu. Mengine yaliyotajwa ni pamoja na wizi mkubwa wa taarifa binafsi, kompyuta kuvamiwa, na aina nyingine za uhalifu mtandao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako