• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raia 17 wauawa katika mapambano yaliyotokea mjini Yei, Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2018-10-17 09:39:25

    Polisi nchini Sudan Kusini wamesema raia wasiopungua 17 wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kwenye mapambano yaliyoibuka kati ya makundi mawili ya waasi katika mji wa mpakani wa Yei, ulioko kusini magharibi mwa Sudan kusini.

    Msemaji wa polisi Bw. Daniel Justine amesema mapambano mapya yaliyotokea kati ya makundi ya waasi ya SPLA-IO na NAS mjini Yei pia yamesababisha raia wengi kukimbia makazi yao.

    Bw. Justine amesema serikali imetoa msaada wa chakula kwa watu waliokimbia mapambano, na jeshi la serikali pia limetakiwa kuchukua tahadhari ya juu kulinda usalama wa raia kwenye eneo hilo.

    Naibu msemaji wa SPLA-IO Bw. Lam Paul Gabriel amevilaani vikosi vya NAS kushambulia kambi yao kwenye maeneo ya Minyori na Logo, na pia ameshutumu vikosi vya serikali katika jimbo la Wau kufanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi yaop kwenye maeneo ya Ngisa, Tado na Ngoku, shutuma ambazo zimekanushwa na msemaji wa jeshi la Sudan kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako