• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China awasili Ubelgiji kwa ziara na kuhudhuria mkutano wa kilele wa ASEM

    (GMT+08:00) 2018-10-17 09:46:11

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amewasili Ubelgiji kwa ziara ya kikazi na kuhudhuria mkutano wa kilele wa 12 wa viongozi wa nchi za Asia na Ulaya (ASEM), ikiwa ni ziara yake ya tatu nchini humo ndani ya miaka minne.

    Bw Li Keqiang amefanya mazungumzo na mwenzake wa Ubelgiji Bw. Charles Michel kuhusu ushirikiano wa pande mbili na umoja wa Ulaya, na kushuhudia kusainiwa kwa waraka za ushirikiano kati ya nchi mbili. Bw Li amependekeza Asia na Ulaya ziimarishe mazungumzo na ushirikiano, ili kupata maendeleo kwa pamoja.

    Kabla ya hapo, waziri mkuu wa Uholanzi Bw Mark Rutte aliahidi kuwa Uholanzi itadumisha uchumi wa ufunguaji mlango, na kutoa wito wa kuanzisha mfumo wa biashara wa dunia wenye usawa, uhuru na uwazi, ili kupinga vitendo vya kujilinda kibiashara. Wakati huo huo, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amekaribisha makampuni ya Uholanzi kwenye soko la China, na kuanzisha ushirikiano mpya wa uvumbuzi na makampuni ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako