• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 19 waliotuhumiwa kuhusiana na kutekwa kwa bilionea wa Tanzania waachiwa huru

    (GMT+08:00) 2018-10-17 09:50:10

    Polisi wa Tanzania wamewaachia huru watu 19 waliotuhumiwa kuhusiana na tukio la kutekwa kwa bilionea kijana Bw. Mohammed Dewji wiki iliyopita.

    Kamanda wa polisi wa kanda maalumu ya Dar es Salaam Bw. Lazaro Mambosasa, amesema watuhumiwa hao 19 waliachiwa baada ya kuhojiwa, lakini wengine 7 bado wanahojiwa.

    Familia ya Bw. Dewji jumatatu ilitangaza donge nono la shilingi bilioni moja za Tanzania kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa kuhusu mtoto wao aliyetekwa. Msemaji wa familia hiyo Bw. Azim Dewji, amesema donge nono hilo linalenga kuimarisha juhudi za kumtafuta bilionea huyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako