• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ahimiza juhudi kushinda kwa wakati vita dhidi ya umasikini

    (GMT+08:00) 2018-10-17 18:19:12

    Rais Xi Jinping wa China ametaka juhudi zaidi ziongezwe katika kushinda vita kali dhidi ya umasikini kwa wakati.

    Rais Xi amesema hayo wakati akitoa maelekezo kuhusu kazi ya kupunguza umasikini wakati China ikiadhimisha Siku ya Tano ya Kupambana na Umasikini inayoangukia Oktoba 17 ya kila mwaka. Rais Xi amesema China inapaswa kushikilia kikamilifu lengo la kuondoa umasikini na kufanya kazi zaidi ili kushinda vita hiyo.

    Wakati huohuo, Ofisi ya Kuondoa Umasikini na Maendeleo iliyo chini ya Kundi la Uongozi la Baraza la Serikali la China imesema kaunti nyingine 85 zimeondolewa rasmi kwenye orodha ya maeneo yenye umasikini uliokithiri, hivyo kuashiria hatua zaidi katika lengo la kuondoa umasikini ifikapo mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako