• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utulivu wa uchumi wa China na soko lake vinaweza kushinda vita ya kibiashara

    (GMT+08:00) 2018-10-17 19:04:04

    Hivi karibuni, Rais Donald Trump wa Marekani alipohojiwa na shirika la utangazaji la Marekani CBS, alisema China haina uwezo wa kulipiza kisasi vita ya kibiashara iliyoanzishwa na Marekani. Wakati huohuo, amedai kuwa kinachotokea kati ya China na Marekani siyo vita ya kibiashara, bali ni mkwaruzano mdogo. Rais Trump amedai kuwa anafikiria kupunguza kiwango cha mkwaruzano huo kati ya nchi hizo mbili.

    Vita ya kibiashara si michezo ya namba, kwani vinahusiana na maslahi ya maelfu ya makampuni na wateja. Serikali ya Marekani imepuuza upinzani wa ndani, na kuongeza zaidi vita ya kibiashara ili kutekeleza sera yake ya "Marekani Kwanza". Lakini serikali ya China haitafuata hatua ya Marekani, pia haitapambana na nchi hiyo bila ya sababu. China siku zote inaweka kipaumbele katika maslahi ya umma, na kulinda kithabiti biashara huria, mfumo wa pande nyingi na maslahi ya pamoja ya nchi mbalimbali. Kwa kutilia maanani maslahi ya umma, uwezo wa kuvumilia wa makampuni na uendeshaji wa mnyororo wa viwanda wa dunia, hatua ya kulipiza kisasi inayochukuliwa na China imelingana na kanuni ya kujizuia, ambayo inalenga kusimamisha vita kupitia vita.

    Ukweli ni kwamba, China kujizuia haimaanishi kuwa risasi zake zimeisha, kinyume chake ni kwamba, ushupavu wa uchumi wa China na soko lake kubwa siku zote vina uwezo mkubwa wa kushinda vita hivyo.

    Kwanza, maendeleo imara ya uchumi wa China yameimarisha uwezo wa kushinda vita hivyo. Jumuiya ya kimataifa imeshudhudia kwamba uchumi wa China umekua kwa asilimia 6.7 hadi 6.9 kwa miaka mitatu mfululizo. Ukuaji wa uchumi wa China umebadilika kutoka kutegemea mauzo ya bidhaa na uwekezaji katika nchi za nje hadi kutegemea zaidi matumizi ya ndani, sekta za huduma na mahitaji ya ndani.

    Pili, duru mpya ya kufungua mlango hasa hatua za kufungua soko itaisaidia China kushinda vita hiyo. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, serikali ya China imeendelea kulegeza vizuizi kwa makampuni ya kigeni kuingia katika soko la China, kulegeza vigezo vya kuingia kwenye soko la China, kuimarisha ulinzi wa hakimiliki ya ujuzi na kupanua kwa hiari uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya China. Utekelezaji wa duru mpya ya sera ya kufunga mlango umevutia mitaji mingi zaidi ya kigeni kuingia nchini China.

    Ikilinganishwa na hali ya China, matokeo ya vita ya kibishara iliyoanzishwa na Marekani yameonesha kuwa nguvu ya Marekani inakaribia kwisha. Hicho ndicho chanzo kikuu kinachomfanya rais Trump kupunguaza mvutano wa kibiashara kati ya China na Marekani kutoka ngazi ya vita hadi ngazi ya mkwaruzano mdogo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako