• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ahimiza kuthamini uhusiano kati ya China na Russia

    (GMT+08:00) 2018-10-17 19:26:32

    Rais Xi Jinping wa China amesema, kutokana na hali ya sasa ya dunia, China na Russia zinapaswa kuthamini zaidi uhusiano mpevu na imara wa kiwenzi kati yao, na kukuza ushirikiano katika sekta mbalimbali kwa kina na bila ya kusitasita.

    Rais Xi ameyasema hayo leo alipokutana na mkurugenzi wa ofisi ya rais ya Russia Bw. Anton Vaino. Amesema hivi sasa uhusiano kati ya nchi hizo mbili ni mzuri zaidi katika historia, pande hizo mbili zinapaswa kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wao kwa haraka, kusukuma mbele kwa kina ushirikiano wa nishati na uvumbuzi, na kuharakisha ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Bw. Vaino amesema Russia inapenda kuongeza ushirikiano na China katika kutekeleza kihalisi makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili, ili kutoa mchango mpya kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kati ya Russia na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako