• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Rwanda na Benki ya AfDB zasaini mkopo wa $269m kuongeza ugavi wa umeme

    (GMT+08:00) 2018-10-17 19:48:04

    Serikali ya Rwanda imeazima $269 million (Rwf237 billion) kutokaBenki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ili kuwekeza katika huduma za umeme endelevu,bei nafuu na hakika.

    Makubaliano ya mkopo huo yalitiwa saini jumanne.Mkopo huo wa masharti utatolewa chini ya awamu ya pili ya mpango wa kuongeza upatikanaji wa umeme,ambao unatarajiwa kuongeza umeme katika gridi ya taifa kwa matumizi ya nyumbani na viwanda.

    Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi Dk Uzziel Ndagijimana,alisema mpango huo utapiga jeki juhudi za serikali za kufikia upatikanaji wa umeme kila sehemu kufikia mwaka 2024.

    Alisema mradi huo utakuwa hatua muhimu katika kuboresha usambazaji wa umeme wa kuaminika,ambao utaleta athari chanya kwa ukuaji wa uchumi,kukuza ukuaji wa utengenezaji wa nafasi za ajira hasa kwa vijana na kupunguza umaskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako