• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yalenga kuteka soko la muhogo China

    (GMT+08:00) 2018-10-17 19:48:24
    Serikali ya Tanzania imewataka wakulima wa zao la muhogo nchini humo kuongeza uzalishaji ili kuwawezesha kupata soko la uhakika nchini China.

    Hatua hiyo itaifanya Tanzania kuongeza wigo wa kusafirisha zao hilo nchini humo ambapo kwa mwaka 2017 inakadiriwa kupeleka bidhaa zenye thamani ya $300,000 (Tsh687m),huku China ikiingiza bidhaa zake nchini Tanzania zenye thamani ya $3.1bn.

    Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Profesa Siza Tumbo,katika mkutano wa wadau wa zao la muhogo kitaifa ambao umeandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI),Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo cha Kitropiki (IITA) ,na Wizara ya Kilimo,kitengo cha Mpango wa Maendeleo wa sekta ya Kilimo awamu ya pili (ASDP II).

    Mkutano unalenga kuandaa mpango wa kuendeleza zao hilo kuwa kibiashara na kuchangia katika maendeleo ya nchi.

    Profesa Siza Tumbo alisema kama taifa kunatakiwa kuwapo na msimamo wa kuchangamkia soko la zao hilo nchini China kutokana na fursa ya kibiashara iliyopo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako