• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda-Bei ya majani chai yashuka kwa miezi mitatu mfululizo

    (GMT+08:00) 2018-10-17 20:01:43

    Bei za majani chai haswa katika wilaya za Bushenyi,Mitooma,Sheema,Rubirizi na Buhweju zimekuwa zikishuka katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita,na kuacha wakulima kukadiria hasara.

    Wakulima hao ambao wengi wao ni wabia wa kiwanda cha wakuzaji chai cha Igara ambacho kina wanachama zaidi ya 7,000,wanaeleza kuwa bei za majani chai zimekuwa zikishuka,kutoka Shs600 mwezi Agosti hadi Shs550 mwezi Septemba na hatimaye Shs470 mwezi huu.

    Wakizungumza katika kikao cha wakulima katika kituo cha Nyakashaka katika wilaya ya Buhweju ,wakulima walisema gharama za uzalishaji zinazidi kuongezeka ukilinganisha na mapato yao.

    Mwakilishi wa Wilaya ya Buhweju ambaye pia ni mkulima wa majani chai ,Bw Mujurizi,alisema kuwa bei zikiendelea kushuka kama inavyoshuhudiwa inamaanisha kuwa mabenki yatachukua mali zao walizoweka kama dhamana ili kupata mikopo ya kufanya kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako