• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Putin asaini makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati na Misri

    (GMT+08:00) 2018-10-18 08:31:54

    Rais Vladimir Putin wa Russia na mwenzake wa Misri Abdel Fattah al-Sisi wamesaini makubaliano kuhusu ushirikiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote kati ya nchi zao katika mji wa Sochi, pwani ya Bahari Nyeusi.

    Rais Putin amepongeza maendeleo mazuri ya uhusiano wa pande mbili katika miaka ya hivi karibuni alipozungumza na mwenzake wa Misri. Kwa upande wake, rais al-Sisi amesema ametilia maanani ushirikiano wa pande mbili katika miradi mikubwa ya pamoja na kusisitiza umuhimu wa juhudi za uratibu na Russia katika kupambana na ugaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako