• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya na Namibia yaweka utaratibu wa pamoja wa kukuza uhusiano wao

    (GMT+08:00) 2018-10-18 09:05:15

    Kenya na Namibia zimeweka utaratibu wa pamoja unaolenga kuhimiza uhusiano kati yao haswa kwenye maeneo ya mashauriano ya kidiplomasia, utalii na mambo ya vijana.

    Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bibi Monica Juma amewaambia wanahabari mjini Nairobi kuwa utaratibu huo ulianzishwa kwenye kikao cha mawaziri cha Mkutano wa uzinduzi wa Kamisheni ya pamoja ya ushirikiano kati ya Kenya na Namibia.

    Bibi Juma amesema utaratibu huo unaotarajiwa kusainiwa wakati wa ziara ya rais Hage Geingob wa Namibia nchini Kenya itakayofanyika Ijumaa wiki hii, utatoa msukumo mkubwa wa kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili ufikie ngazi ya kimkakati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako