• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR yahitaji fedha zaidi kuwahudumia wakimbizi zaidi ya laki 9 nchini Ethiopia

    (GMT+08:00) 2018-10-18 09:05:32

    Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR limetoa wito kwa dunia kuchangia fedha zaidi kwa ajili ya kutoa misaada kwa wakimbizi zaidi ya laki tisa nchini Ethiopia.

    Taarifa iliyotolewa na UNHCR inasema hadi kufikia Septemba 11, Shirika hilo lilikuwa limepokea dola milioni 69.5 za kimarekani tu, ikilinganishwa na dola 327.8 zinazohitajika kufikia mahitaji ya msingi ya wakimbizi nchini Ethiopia kwa mwaka huu.

    UNHCR pia imesema inapokea wakimbizi wengi kutoka Eritrea walioingia Ethiopia baada ya kufunguliwa tena kwa mipaka kati ya nchi hizo mbili, hali inayoufanya wito wake wa kuchangiwa fedha, uwe wa dharura zaidi.

    Imefahamika kuwa mbali na wakimbizi hao milioni tisa kutoka nje, bado kuna wakimbizi milioni 2.8 wa ndani nchini Ethiopia wanaohitaji misaada ya kibinadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako