• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa mwito wa kukata vyanzo vya fedha na silaha kwa magaidi nchini Syria

    (GMT+08:00) 2018-10-18 09:05:58

    Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kufanya juhudi za pamoja kukata vyanzo vya fedha na silaha kwa makundi ya kigaidi nchini Syria.

    Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la usalama kuhusu suala la Syria, Bw. Ma Zhaoxu amesema mchakato wa kisiasa nchini Syria umekuwa na mwelekeo chanya, na makubaliano ya kutuliza hali na kukomesha mapambano kwenye eneo la Idlib yaliyosainiwa na Uturuki na Russia yametekelezwa vizuri. Lakini pia ameongeza kuwa mchakato huo bado unakabiliwa na changamoto za kigaidi, zinazotishia usalama na utulivu nchini Syria, na kuzuia ukarabati na kurudi kwa wakimbizi.

    Habari nyingine zinasema, wajumbe wa Umoja wa Ulaya katika Baraza la usalama la Umoja wa mataifa wamezitaka pande zote za kisiasa nchini Syria, haswa serikali, kushirikiana kwa ajili ya kuunda mapema kamati ya katiba iliyo shirikishi na yenye kuaminika, ili kuendeleza juhudi zilizofanywa na Umoja wa Mataifa kutimiza ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro wa Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako