• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa Uturuki wafanya upekuzi kwenye ubalozi wa Saudi Arabia kuhusiana na mwanahabari aliyepotea

    (GMT+08:00) 2018-10-18 09:19:46

    Maofisa wa Uturuki jana waliingia kwenye makazi ya ofisi ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Istanbul, kutafuta ushahidi zaidi kuhusiana na mwanahabari wa Saudi Arabia aliyepotea Jamal Kashoggi.

    Maofisa wa polisi na wachunguzi wa maeneo ya matukio ya uhalifu CSI walifika kwenye makazi ya Konsela mkuu wa ubalozi wa Saudi Arabia Bw. Mohammed al-Otaibi, aliyeondoka kurudi Saudi Arabia siku moja kabla, akiwa na msafara wa magari 15 ikiwa ni pamoja na mabasi madogo matano.

    Wachunguzi wa Uturuki wamefanya upekuzi kwa muda wa saa tisa kwenye jengo hilo, na vyombo vya habari vya huko vimeripoti kuwa kuna "ushahidi kiasi" uliopatikana, kuwa mwanahabari huyo aliuawa ndani ya jengo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako