• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika walaani kusimamishwa kwa mazungumzo ya kuleta masikilizano kati ya waComoro

    (GMT+08:00) 2018-10-18 09:20:09

    Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Mahamat, amelaani kusimamishwa kwa mazungumzo ya kuleta masikilizano kati ya wanasiasa wa Comoro.

    Bw. Mahamat amesema hayo wakati mazungumzo ya masikilizano ya Comoro, yaliyoanza septemba 14 chini ya upatanishi wa Kamishna mkuu wa Umoja wa Afrika Bw. Ramtane Lamamra, yalikuwa yamesimamishwa hadi kufikia Oktoba 2.

    Umoja wa Afrika umesema kudorora kwa hali ya kisiasa nchini Comoro, kunatokana na kuondolewa kwa kinga ya bunge kwa wabunge watatu wa nchi hiyo, kulikofanywa tarehe 3 Oktoba. Watu hao waliovuliwa kinga ni sehemu ya wawakilishi wa wapinzani kwenye mazungumzo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako