• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya dunia yatoa mwito wa uwekezaji zaidi katika kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa Afrika

    (GMT+08:00) 2018-10-18 09:20:32

    Benki ya dunia imetoa mwito wa kuongeza uwekezaji kwenye teknolojia ya kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa, hasa kwa nchi za Afrika. Akiongea nchini Zambia anakofanya ziara ya siku tatu, makamu mkuu wa Benki ya dunia Bw Hafez Ghanem, amesema uwekezaji kwenye uwezo wa kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa, ni jambo muhimu kwa kuwa mabadiliko ya hali ya hewa ni tishio kwa sekta ya kilimo na usalama wa chakula barani Afrika.

    Akiongea baada ya kukutana na waziri wa fedha wa Zambia Bibi Margaret Mwanakatwe, Bw Ghanem amesema benki ya dunia inaisaidia Zambia kutekeleza miradi mbalimbali yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.2 ambazo ni mkopo kutoka shirika la kimataifa la misaada ya maendeleo IDA.

    Amesema msaada wa IDA kwa Zambia ambao umekuwa ukiendelea kwa mwaka mmoja na nusu sasa, ulijikita zaidi kwenye kuwawezesha wasichana na wanawake, afya na kupatikana kwa umeme.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako