• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan asisitiza ufuatiliaji wake juu ya mchakato wa amani nchini Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2018-10-18 09:39:06

    Rais Omar al-Bashir wa Sudan amesisitiza kuwa nchi hiyo inafuatilia mchakato wa amani wa Sudan Kusini.

    Akiongea na wafanyakazi wa wizara ya mambo ya nje ya Sudan, Rais al-Bashir amesema, amani ya Sudan haiwezi kutenganishwa na amani katika eneo hilo, na kwamba anaamini kuwa upatikanaji wa amani nchini Sudan Kusini ni hatua kubwa katika kutafuta amani ya kudumu na ya pande zote nchini Sudan.

    Rais al-Bashir pia ametangaza uteuzi wa Bw. Jamal Al-Sheikh kuwa mjumbe wake maalumu nchini Sudan Kusini, kwa kufuata utekelezaji wa makubaliano ya amani nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako