• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi tatu za Afrika Mashariki zatafuta kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia

    (GMT+08:00) 2018-10-18 09:39:31

    Nchi tatu za Afrika Mashariki zimesisitiza nia zao za kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia kwa ajili ya amani na utulivu katika eneo hilo.

    Mawaziri wa mambo ya nje wa Ethiopia, Somalia na Eritrea, waliofanya mazungumzo mjini Mogadishu, Somalia, wamesisitiza kuwa utulivu katika eneo hilo unategemea maafikiano ya viongozi wao.

    Taarifa ya pamoja iliyotangazwa baada ya mazungumzo yao, inasema mawaziri hao wamejadili maendeleo yaliyopatikana katika utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande hizo tatu kuhusu ushirikiano katika sekta za uchumi, siasa na amani, pia wamesisitiza kuwa wataendelea kuchangia mchakato wa amani, utulivu na maendeleo katika Pembe ya Afrika.

    Pia wamesema mkutano huo ni sehemu ya ushirikiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo tatu na mchakato wa mazungumzo unaoendelea kwa kufuata makubaliano yaliyofikiwa kati ya nchi hizo tatu mwezi Septemba, huko Asmara, Eritrea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako