• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Ubelgiji zaimarisha ushirikiano

    (GMT+08:00) 2018-10-18 09:40:12

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ambaye yuko ziarani nchini Ubelgiji, amesema China iko tayari kuimarisha ushirikiano na Ubelgiji katika ngazi zote. Akiongea na mwenzake wa Ubelgiji Bw. Charles Michel, Bw Li amesema uhusiano kati ya China na Ubelgiji unadumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo, na kampuni za Ubelgiji zinakaribishwa kuwekeza nchini China, hali ambayo itatoa fursa zenye usawa kwa kampuni zote za China na za kigeni.

    Naye Bw. Michel amesema Ubelgiji iko tayari katika kuoanisha mpango wa mafungamano wa Umoja wa Ulaya na Pendekezo la China la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kuunga mkono kampuni za Ubelgiji kuwekeza nchini China.

    Mawaziri hao wawili pia wamekubaliana kuendelea na ushirikiano wa kunufaishana, kupanua maeneo ya ushirikiano, na kuhimiza maendeleo mapya katika ushirikiano wenye ufanisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako