• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wadhamiria kushirikiana na Umoja wa Afrika katika kutatua masuala ya Afrika

    (GMT+08:00) 2018-10-18 10:00:52

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa ahadi yake ya kushirikiana na Umoja wa Afrika katika kutatua masuala ya Afrika.

    Bw Guterres akihudhuria ufunguzi wa mkutano wa Mazungumzo kuhusu mambo ya Afrika wa mwaka huu, yanayolenga kuhamasisha dunia kuunga mkono maendeleo ya Afrika, amesema Umoja wa Mataifa unawaamini viongozi wa nchi za Afrika katika kutatua masuala ya Afrika, pia unadhamiria kushirikiana na Umoja wa Afrika kwa kushikamana na kuheshimiana, ili kutumia vizuri uwezekano mkubwa unaoletwa na fursa za hivi leo.

    Ameongeza kuwa makubaliano mawili yaliyosainiwa na pande hizo mbili miezi 18 iliyopita, ikiwa ni pamoja na Ajenda ya maendeleo endelevu ya kuelekea mwaka 2030 na Ajenda ya mwaka 2063 ya Afrika, yamekuwa msingi wa ushirikiano mpya kati ya pande hizo mbili, ambayo yanatoa wito wa kuifanya Afrika iwe bara lenye ustawi, amani na usalama kwenye msingi wa haki za binadamu, utawala bora na utawala wa kisheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako