• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya mji wa Wenzhou yahimiza kampuni binafsi kuendelea vizuri

    (GMT+08:00) 2018-10-18 18:13:35

    Serikali ya mji wa Wenzhou wa mkoa wa Zhejiang hivi karibuni iliandaa shughuli mbalimbali za kuhimiza kampuni binafsi kuendelea vizuri. Ukiwa mji ulioanza kuwa na kampuni binafsi mapema zaidi nchini China, mji huo utabeba majukumu ya kuwa "mvumbuzi" na "mtangulizi" tena katika mageuzi ya kampuni binafsi.

    Katika miaka 40 iliyopita tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, kampuni binafsi nchini China zimezalisha asilimia zaidi ya 60 ya mali ya taifa kwa kutumia asilimia 40 ya rasilimali, na kutoa zaidi ya asilimia 80 ya ajira. Hivi sasa uchumi wa China uko katika kipindi muhimu cha kubadilisha njia ya kujiendeleza. Kutokana na hali ya kutatanisha ya uchumi wa dunia, haswa kuongezeka kwa mikwaruzano ya biashara, kampuni binafsi ambazo zinachangia asilimia 45 ya mauzo katika nchi za nje zinakabiliwa na changamoto kubwa, na zinahitaji sana kuungwa mkono na serikali. Rais Xi Jinping hivi karibuni alipokwenda kukagua mkoa wa Liaoning alisisitiza umuhimu wa kuanzisha mazingira mazuri ya kisheria na kibiashara kwa ajili ya kampuni binafsi.

    Katika miaka mingi iliyopita, mji wa Wenzhou umekuwa mtangulizi katika kuvumbua njia mpya ya kuendeleza kampuni binafsi. Takwimu zinaonesha kuwa asilimia 10 ya watu wa mji huo wana kampuni, na kampuni binafsi zinachukua asilimia 99.5 ya kampuni zote mjini huo. Hivyo kuufanya mji huo kuwa ni sehemu ya kufanyia majaribio ya kuendeleza kampuni binafsi ni hatua muhimu ya kuhimiza ustawi wa kampuni binafsi kote nchini China.

    Hivyo serikali ya mji wa Wenzhou imepanga kuboresha mazingira ya biashara mjini humo kuwa bora zaidi nchini China ndani ya miaka mitatu, na kujenga mfumo wa kisasa wa uchumi unaolingana na mahitaji ya zama mpya hadi kufikia mwaka 2025. Mbali na hayo, mji huo pia utaanzisha mazingira mazuri zaidi kwa ajili ya kampuni binafsi ndogo na zenye ukubwa wa kati, na kupunguza mizigo na vizuizi vya kuingia sokoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako