• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan iko tayari kuendelea na mazungumzo na wapinzani na makudi yenye silaha

    (GMT+08:00) 2018-10-18 18:33:44

    Serikali ya Sudan imeeleza kuwa iko tayari kuanza tena mazungumzo na upande wa upinzani na makundi yenye silaha.

    Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazungumzo kati yake na kiongozi wa Tume ya Ngazi ya Juu ya Utekelezaji ya Umoja wa Afrika kuhusu Sudan Thabo Mbeki mjini Khartoum hapo jana, msaidizi wa rais wa nchi hiyo Faisal Hassan Ibrahim amesema, mazungumzo yao yalilenga masuala yanayohusiana na ushiriki wa pande zinazohusika na muswada wa makubaliano uliopendekezwa na Umoja wa Afrika kuhusu maandalizi ya katiba ya Sudan na sheria ya uchaguzi.

    Pia amesema walijadili matokeo ya mkutano kati ya Bw. Mbeki na wakuu kadhaa wa upande wa upinzani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako