• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yapata msaada wa fedha za kuhamisha njia ya reli kwenye mpaka kati yake na Sudan Kusini na DRC

    (GMT+08:00) 2018-10-18 18:34:09

    Uganda imepata msaada wa dola za kimarekani milioni 24.88 kutoka Umoja wa Ulaya utakaosaidia kuhamisha kilomita 375 za njia ya reli kutoka mji wa Tororo ulioko eneo la mpaka wa mashariki kwenda wilaya ya kaskazini ya Gulu.

    Waziri wa Fedha wa Uganda Matia Kasaija na kiongozi wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Uganda balozi Attilio Pasifici walisaini makubaliano ya msaada huo jana mjini Kampala.

    Njia ya reli ya Tororo-Gulu ilikuwa muhimu sana kiuchumi katika ushoroba wa kaskazini wa Afrika Mashariki, ikiunganisha bandari ya Mombasa nchini Kenya na eneo la mashariki na kaskazini mwa Uganda, na pia nchi jirani ya Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako