• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mitaji ya kigeni inayovutiwa na China katika robo tatu za mwanzo za mwaka huu yaongezeka kwa utulivu

    (GMT+08:00) 2018-10-18 19:19:03

    Takwimu zilizotolewa na wizara ya biashara ya China zimeonesha kuwa mwezi wa Januari hadi Septemba mwaka huu, China imetumia mitaji ya kigeni dola bilioni 91.8 za kimarekani, ambayo imeongezeka kwa asilimia 2.9 ikilinganishwa na ya mwaka jana.

    Msemaji wa wizara hiyo Bw. Gao Feng amesema, matumizi ya mitaji ya kigeni katika sekta ya utengenezaji wa bidhaa za teknolojia ya ubora wa juu yameongezeka kwa kasi zaidi. Sekta hiyo imetumia mitaji ya kigeni ya dola bilioni 9.3 za kimarekani, ambayo imeongezeka kwa asilimia 22.5 ikilinganishwa na ya mwaka jana.

    Kwa mujibu wa takwimu za robo tatu za mwanzo za mwaka huu, mitaji kutoka Korea Kusini, Japani na Uingereza imedumisha ongezeko la kasi, huku mitaji kutoka nchi za "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ikiongezeka kwa asilimia 14.9.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako