• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Safaricom yapandisha ada za mawasiliano

    (GMT+08:00) 2018-10-18 20:26:53

    Sasa wakenya watalazimika kutenga fedha za ziada kwa ajili ya mawasiliano.

    Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom nchini Kenya imeongeza ada za mawasiliano kufuatia ongezeko la asilimia 15 ya ushuru wa bidhaa.

    Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo nchini Kenya Bob Collmore, amearifu kuwa ada za kupiga simu zitaongezeka kwa senti 30 na pia mteja atalipia senti 10 zaidi za kutuma ujumbe kuanzia leo.

    Bei hizi mpya zimethibitishwa na halmashauri ya mawasiliano nchini Kenya kwa mujibu wa sheria mpya ya ushuru.

    Sheria mpya ya ushuru imeongeza ushuru wa bidhaa za mafuta kwa asilimia 8, jambo lililopelekea kupandishwa bei kwa bidhaa muhimu nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako