• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Marufuku waganda kusafiri Oman kwa ajira

    (GMT+08:00) 2018-10-18 20:26:53

    Serikali ya Uganda imepiga marufuku na kusitisha mara moja safari za waganda nchini Oman kutafuta ajira .

    Marufuku haya yanajiri kufuatia uchunguzi ulioanzishwa dhidi ya visa vya ukandamaziji wa haki raia wa Uganda nchini Oman.

    Wiki iliyopita, wanawake 15 raia wa Uganda wanadaiwa kutaka kusafarishwa nchini Jordan kwa ulanguzi wa binadamu.

    Visa kadhaa vya mateso ,ubakaji na ukatili kwa wafanyikazi wa nyumbani ama mayaya kutoka Uganda aidha vimeripotiwa nchini Oman .

    Waziri wa jinsia nchini Uganda Janat Mukwaya ,amesema baadhi ya kampuni feki huajiri waganda kwa kazi za nyumbani na madukani na badala yake huwatumia kwa njia tatanishi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako