• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Wafanyibiashara kupata merejesho ya fedha

    (GMT+08:00) 2018-10-18 20:29:58

    Wafanyibiashara jijini Daresalaam wameendelea kupokea marejesho ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT Refund) kutoka kwa serikali.

    Hii ni baada ya serikali kuahidi marejesho hayo mwezi uliopita kwa kampuni na wafanyabiashara mbalimbali nchini Tanzania wakiwemo waagizaji wa sukari za viwandani.

    .

    Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpangoamesema kuchelewa kulipwa kwa madai hayo kunatokana na kuwepo kwa udanganyifu mkubwa kwa baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu hivyo kutaka kuingizia Serikali hasara kwa kulipa madai hewa.

    Pia amesema Serikali inalifanyia kazi suala la mazingira ya kufanyia biashara na wingi wa kodi anazolipa mfanyabiashara kwa taasisi mbalimbali za serikali ili kodi hizo ziweze kutozwa sehemu moja na kupunguza adha wanazopata walipa kodi.

    Lakini ili Serikali itekeleze wajibu wake, wafanyabiashara wametakiwa kushiriki katika mikutano ya sera za kodi inayondaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango ambayo huanza mwezi Disemba hadi Januari kila Mwaka ili kutengeneza mizania ya ulipaji kodi nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako