• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan ahimiza upinzani kushiriki kwenye utungaji wa katiba na uchaguzi

    (GMT+08:00) 2018-10-19 09:54:49

    Rais Omar al-Bashir wa Sudan amevihimiza vyama vya upinzani kushiriki kwenye utungaji wa katiba na maandalizi ya uchaguzi mkuu, unaotarajiwa kufanyika mwezi Aprili mwaka 2020.

    Rais al-Bashir amesema hayo alipokutana na mkurugenzi wa Jopo la Ngazi ya juu la utekelezaji la Umoja wa Afrika AUHIP Bw. Thabo Mbeki. Pia amesisitiza kuwa serikali yake itaendelea na mazungumzo na vyama vyote, ili kuwashirikisha wananchi wote wa Sudan katika ujenzi wa taifa.

    Kwa upande wake Bw. Mbeki amesema juhudi za serikali za kutafuta ufumbuzi wa kudumu na nia yake ya kushirikisha vyama vyote kwenye mazungumzo, vimetoa motisha kwa wasuluhishi kuendelea na juhudi za kutimiza amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako