• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan kusini yaipongeza Sudan kuteua mjumbe maalumu wa amani

    (GMT+08:00) 2018-10-19 09:55:07

    Sudan kusini imekaribisha uteuzi uliofanywa na serikali ya Sudan wa Bw. Jamal El-Sheikh kuwa mjumbe maalumu kuhusu mchakato wa amani wa Sudan Kusini.

    Msemaji wa rais wa Sudan Kusini Bw. Ateny Wek Ateny amesema Bw. El-Sheikh anafahamu vizuri pande mbalimbali za kisiasa kwa upande wa serikali na wa makundi ya waasi, ambao utasaidia utekelezaji wa makubaliano ya amani yaliyosainiwa hivi karibuni kati ya pande hasimu nchini Sudan kusini.

    Naye naibu mkurugenzi wa habari na mahusiano wa SPLM/A-IO Bw. Puok Both Baluang, ameeleza kufurahishwa na uteuzi huo na kuahidi kuwa watashirikiana na Bw. El-Sheikh kutekeleza makubaliano ya amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako