• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China Bw Li Keqiang akutana na wenzake wa Vietnam na Cambodia

    (GMT+08:00) 2018-10-19 10:34:51

    Waziri mkuu wa China Bw Li Keqiang jana alikutana na mwenzake wa Vietnam Bw Nguyen Xuan Phuc kwenye mkutano wa kilele wa viongozi wa Asia na Ulaya unaofanyika mjini Brussels, Ubelgiji.

    Bw Li amesema China na Vietnam ni majirani wema na wenzi wazuri wa ushirikiano wa kunufaishana. Amesema China inapenda kuhimiza ushirikiano na Vietnam katika sekta mbalimbali.

    Bw Nguyen Xuan Phuc amesema Vietnam inapenda kuhimiza biashara na China na kutaka iendelee kukua kwa uwiano, na amekaribisha makampuni ya China kujenga eneo la viwanda nchini Vietnam.

    Bw Li Keqiang pia amekutana na mwenzake wa Cambodia Bw Hun Sen. na kusema nchi hizo mbili zinapaswa kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kibiashara. Bw Hun Sen amesema Cambodia inapenda kuimarisha ushirikiano na China kwenye mambo ya kimataifa na ya kikanda, na kupanua ushirikiano kwenye sekta za biashara na kilimo.

    Mbali na hayo, Bw Li Keqiang jana ametembelea kituo cha utafiti wa mikroelectroniki cha Ubelgiji mjini Leuven. Mkurugenzi wa kituo hicho ameeleza kwamba kituo chake kimeshirikiana na China katika kufanya makongamano ya kitaaluma na mafunzo kwa wataalamu, na kinapenda kupanua uhusiano wa ushirikiano na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako