• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa China waongezeka kwa asilimia 6.7 katika robo tatu zilizopita mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-10-19 16:41:56

    Idara ya takwimu ya China leo imetoa takwimu ikionesha kuwa, katika robo tatu zilizopita mwaka huu, thamani ya uzalishaji wa mali nchini China iliongezeka kwa asilimia 6.7 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Msemaji wa idara hiyo Bw. Mao Shengyong amesema uchumi wa China umeendelea kwa utulivu, na kudumisha mwelekeo mzuri.

    Takwimu zilizotolewa na idara ya takwimu ya China zinaonesha kuwa, katika robo tatu zilizopita, thamani ya uzalishaji mali nchini China ilikuwa karibu dola trilioni 9.37 za kimarekani, na kuongezeka kwa asilimia 6.7 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Msemaji wa idara ya takwimu ya China Bw. Mao Shengyong amejumuisha hali ya uchumi wa China kwa sentensi tatu. Anasema,

    "Kwanza, hali ya utulivu haijabadilika. Pili, maendeleo mfululizo yamedumu. Na tatu, injini mpya imekua kwa haraka."

    Msemaji huyo amesema, katika robo tatu zilizopita mwaka huu, ajira mpya mijini zimeongezeka kwa zaidi ya milioni 11, ambalo ni lengo la mwaka mzima. Licha ya chakula na nishati, mfumuko wa bei ya bidhaa nyingine ulikuwa asilimia 2, ambayo ni sawa na nusu ya kwanza ya mwaka huu. Wakati huo huo pato la watu pia liliongezeka kwa asilimia 6.6.

    Mtafiti wa kituo cha utafiti wa maendeleo cha baraza la serikali la China Bw. Zhang Liqun anaona kuwa, ingawa kasi ya ongezeko la viwanda ilishuka katika robo tatu zilizopita, huku kasi ya kukua kwa uchumi ikishuka katika robo ya tatu, lakini mwelekeo mzuri wa maendeleo ya uchumi wa China haujabadilika. Anasema,

    "Mwaka huu uwekezaji unaolingana na mahitaji ya soko umerejea kuwa tulivu. Uwekezaji katika sekta za uzalishaji viwandani, nyumba na uwekezaji wa watu binafsi umedumu kuwa na kiwango cha juu, na kiasi cha kupungua kwa kasi ya ongezeko la uwekezaji wa miundombinu pia kimepungua. Licha ya hayo, kasi ya ongezeko la matumizi ya ndani iliyoshuka kati ya Januari hadi Julai mwaka huu imeongezeka tena katika miezi ya Agosti na Septemba."

    Hata hivyo, Bw. Mao amesema maendeleo ya China yanakabiliwa na mabadiliko ya hali ya nje, katika robo tatu zilizopita, injini ya maendeleo ya uchumi wa dunia na biashara ya kimataifa imepungua, hali hii pamoja na msukosuko wa fedha katika baadhi ya nchi na mkwaruzano wa kibiashara kati ya China na Marekani, maendeleo ya uchumi wa China yanakabiliwa na changamoto nyingi. Lakini anaona kuwa, uchumi wa China ni imara, na hali ya jumla ni nzuri. Anasema,

    "China ina mazingira, uwezo na imani kutimiza lengo la kuendeleza uchumi kwa asilimia 6.5 kwa mwaka huu. Mwakani uchumi utakabiliwa zaidi na hali ya kutatanisha ya nje, lakini tukijishughulisha vizuri na mambo ya ndani, tutaweza kudumisha utulivu wa maendeleo ya uchumi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako