• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • BancABC yazindua kadi maalum kwa wafanya biashara wanaokwenda China

    (GMT+08:00) 2018-10-19 20:29:49

    Benki ya BancABC imerahisisha miamala ya Watanzania wanaotembelea China kwa kuanzisha kadi maalumu ya malipo . Tangazo hilo linakuja wakati ambapo biashara kati ya China na Tanzania imekuwa ikiimarika., Kadi hiyo ya kabla inayojulikanayo Yuan pre-paid Visa card inawawezesha wafanyabiashara kufanya malipo kwa sarafu za China.

    Mkuu wa kitengo cha dijitali cha BancABC, Silas Matoi amesema China ni kati ya nchi kubwa inayofanya biashara na mataifa mengi duniani ikiwamo Tanzania ambayo ina zaidi ya wanafunzi 6,000 wanaosoma nchini humo hivi sasa.

    Kadi hiyo pia ina huduma ya kupokea ujumbe mfupi wa maneno kumpa mmiliki taarifa za kila muamala anaofanya mtandaoni na haina makato ya mwezi.

    Mkurugenzi wa kitengo cha wateja binafsi na wafanya biashara wa benki hiyo, Joyce Malai amesema kuzinduliwa kwa kadi hiyo ni mwendelezo wa huduma bora na zenye kutoa suluhisho kwa wateja.

    Kadi hiyo inayopatikana kwa saa 24 kwa siku saba za wiki, inaweza kutumika kwenye zaidi ya mashine milioni 2.7 za kutolea fedha (ATM) zinazopokea kadi za Visa duniani kote pamoja na maduka milioni 46. Nchini Tanzania kuna ATM 400 na maduka 1,000 yanayokubali kadi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako