• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wabunge Kenya wataka bidhaa za wafanya biashara wadogo kuachiliwa

    (GMT+08:00) 2018-10-19 20:30:44

    Wabunge nchini Kenya wameitaka serikali kuingilia kati ili bidhaa za wafanyabiashara wa Kenya zenye thamani ya shilingi bilioni 12 zilizozuiliwa katika Bandari ya Mombasa ziachiliwe.

    Wabunge hao wameitaka Serikali Kuu kuamuru kuachiliwa kwa bidhaa hizo zilizoagizwa kutoka nje na wafanyabiashara wadogo wadogo.

    Bidhaa hizo ziliagizwa na wafanyabiashara hao kutoka mataifa ya ng'ambo na zimekua zikizuiliwa katika bandari ya Mombasa kwa miezi miwili kwa madai kuwa ni ghushi.

    Wamelaumu mashirika ya serikali kama vile Mamlaka ya Ukusanyaji wa Ushuru Nchini (KRA) na Shirika la Kupambana na Bidhaa Feki (Kebs) kwa kuwapendelea wafanyabiashara matajiri na kupuuzilia mbali masilahi ya wafanyabiashara wadogo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako