• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sheria za Michuki kuanza kufanya kazi Kenya

    (GMT+08:00) 2018-10-19 20:31:04

    Maelfu ya magari ya uchukuzi wa umma yataondolewa barabarani kwenye operesheni kubwa itakayoanza Novemba 1, 2018.

    Operesheni hiyo inalenga madereva, makondakta, polisi wa trafiki, wenye magari na kampuni za kujenga magari ili kurejesha kikamilifu "Sheria za Michuki".

    Wiki hii Serikali inatarajiwa kutangaza sera na kanuni mpya, na kuwapa wahudumu hadi Novemba 1, 2018 kuhakikisha wametekeleza kanuni hizo ikiwemo mikanda ya usalama, vidhibiti kasi na sare rasmi kwa madereva na makodkta.

    Sasa pia itakuwa lazima kwa mashirika ya matatu na mabasi (Sacco) kuwapa ajira ya kudumu madereva, makodakta, mainspekta na mekanika wa magari yanayosimamia.

    Operesheni hiyo pia inatarajiwa kuzima shughuli za magenge yanayosimamia sekta hiyo ya thamani ya mabilioni ya pesa.

    Madereva wote wa matatu na makanga watakaguliwa upya kuhakikisha ni wale tu waliotimiza sheria za NTSA wanaoruhusiwa kuendesha magari ya kubeba abiria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako