• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan na Umoja wa Mataifa zasaini makubaliano ya kuwaunga mkono wakimbizi wa Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2018-10-22 09:27:12

    Tume ya wakimbizi ya Sudan imetoa taarifa ikisema kuwa Sudan na Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP jana walisaini makubaliano yenye thamani ya dola milioni 21 za kimarekani kwa ajili ya kuiunga mkono jamii ya wakimbizi wa Sudan Kusini iliyoko jimbo la White Nile nchini Sudan.

    Kwa mujibu wa taarifa makubaliano hayo yatatekelezwa kwa awamu tatu. Awamu ya kwanza ilizinduliwa jana kwa kuipatia jamii hiyo ya wakimbizi mashine na vifaa vyenye thamani ya dola milioni 2.2 za kimarekani, vikiwemo matrekta, mashine za kuvunia na pampu za maji.

    Kamishna anayeshughulikia mambo ya wakimbizi nchini Sudan Bw Hamad Al-Jizouli amesema kuwa mambo muhimu zaidi ni kurudisha miradi ya kilimo, na kuwapatia nishati ya umeme na mashamba ya kulima. Ameongeza kuwa hivi sasa wakimbizi zaidi ya laki 1.5 wa Sudan Kusini wamepokewa jimboni White Nile nchini Sudan, na wengine zaidi ya elfu 88 wako miji mingine iliyoko karibu na jimbo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako