• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wahamiaji zaidi ya 13,000 warudishwa kwa hiari nchini kwao kutoka Libya katika mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2018-10-22 09:47:58
    Wahamiaji zaidi ya 13,000 warudishwa kwa hiari nchini kwao kutoka Libya katika mwaka 2018

    Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Libya imesema, wahamiaji zaidi ya 13,000 wameondoshwa Libya na kurudishwa kwa hiari katika nchi zao na Shirika la Kimataifa la Wahamiaji IOM katika mwaka 2018.

    Tume hiyo imesema, hatua hii ni sehemu ya mpango wa IOM wa kuwarudisha wahamiaji kwa hiari, unaolenga kuwarudisha wahamiaji haramu waliokwama nchini Libya katika nchi zao.

    Kambi za wahamiaji nchini Libya zimejaa maelfu ya wahamiaji waliookolewa au kukamatwa na Idara ya usalama ya Libya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako