• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya chakula kwa shule za Tunisia kuunga mkono utoaji wa lishe bora kwa watoto

    (GMT+08:00) 2018-10-22 09:48:27

    Waziri wa Elimu wa Tunisia Bw. Hatem Ben Salem amesema, kuanzishwa kwa Benki ya chakula katika shule kutahimiza utaratibu wa chakula shuleni na kuongeza ubora wake.

    Akihutubia ufunguzi wa Mkutano wa 20 wa Baraza la utoaji wa lishe bora kwa watoto la Dunia uliofanyika huko Tunis na kuhudhuriwa na waziri mkuu wa Tunisia Bw. Youssef Chahed pamoja na wajumbe 300 kutoka nchi 50, Bw. Salem amesema wanatafuta utaratibu wa pamoja na vyombo vya kusimamia lishe ya watoto. Amesema mbali na uungaji mkono wa serikali, fedha za benki hiyo zitakusanywa kutoka sekta binafsi na asasi za kiraia.

    Mkurugenzi mtendaji wa baraza hilo Bibi Arlene Mitchell amesema, wajumbe wanajadili masuala kuhusu lishe ya watoto kote duniani, ili kuhimiza ushirikiano kati ya nchi mbalimbali na kuhimiza nchi hizo kuendeleza na kuboresha mipango ya utoaji wa lishe kwa shule ambayo inachangia katika kutafuta maendeleo endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako