• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya Afrika Mashariki yapongeza uteuzi wa Raila Odinga kama Mwakilishi wa Umoja huo

    (GMT+08:00) 2018-10-22 10:14:55

    Jumuiya ya Afrika Mashariki jana ilipongeza uteuzi wa kiongozi wa upinzani wa Kenya Raila Odinga kama Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Afrika atakayeshughulikia Maendeleo ya Miundo Mbinu katika Afrika.

    Kwenye taarifa yake, Katibu Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Kiserikali la nchi za Afrika Mashariki IGAD Mahboub Maalim, amesema jukumu muhimu la maendelo ya miundo mbinu ni kichocheo kikubwa cha maendeleo endelevu ya uchumi, na kusisitiza kuwa anatambua uongozi wa busara, uzoefu mkubwa, elimu na ujuzi wa Bw. Raila. Amefafanua kuwa jukumu hili litahamasisha juhudi za pamoja katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Miundo Mbinu wa Afrika PIDA, na kusisitiza kuwa mpango huo ni uti wa mgogo wa Ajenda ya mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika.

    Naye Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amesema Bw. Odinga atasaidia na kuimarisha juhudi za idara husika za kamisheni hiyo pamoja na Mashirika ya Mipango na Uratibu wa Ushirikiano Mpya wa Maendelo ya Afrika NEPAD, ndani ya mwongozo wa PIDA, uliopitishwa na baraza kuu la Jumuiya hiyo Januari 2012.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako