• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China bara yatuma salamu za rambirambi kutokana na ajali ya treni huko Taiwan

    (GMT+08:00) 2018-10-22 16:10:14

    Mamlaka za China bara leo zimeomboleza watu waliofariki katika ajali ya treni iliyoacha njia huko Taiwan jana jioni, na kutoa salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa na kuwatakia heri majeruhi.

    Maofisa kutoka Ofisi ya Masuala ya Taiwan iliyo chini ya Baraza la Serikali la China na Jumuiya ya Uhusiano katika Ushoroba wa Taiwan wamesema, China bara inafuatilia kwa makini ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 18 na wengine 187 kujeruhiwa.

    Treni hiyo namba 6432 ilikuwa ikielekea Taitung kutoka kituo cha Shulin ikiwa na abiria 366, na iliacha njia jana jioni katika kituo cha treni cha Xinma, kaunti ya Yilan.

    Chanzo cha ajali hiyo bado kinaendelea kuchunguzwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako