Rais Yoweri Kaguta Museveni amezindua rasmi ujenzi wa daraja la mita 525 litakaloitwa darala la mto Nile katika eneo la Jinja Uganda.
Daraja hilo la gharama ya dola milioni 112 litajengwa na kampuni ya Japan.
Kwa mujibu wa wanauchumi,daraja hilo litatumika pakubwa katika kurahisisha uchukuzi wa bidhaa kuingia na kutoka Uganda hadi Kenya jambo litakaloimarisha uchumi.
Zaidi ya watu 800 watahusika katika ujenzi wa daraja hilo litakalokuwa la pili kwa ukubwa baada ya lile ya Kigamboni la Tanzania.
Daraja hili pia litatumika kuvutia watalii na wahandisi wanasema, litaweza kudumu kwa kwa zaidi ya miaka 120.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |