• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan:Miradi ya chakula na maendeleo yapewa kipau mbele

    (GMT+08:00) 2018-10-22 20:19:02

    Wizara ya kilimo nchini Sudan imetangaza kuzingatia miradi ya kilimo,ajira na maendeleo ili kukabiliana na umaskini nchini humo.

    Sudan imeahidi kushirikiana na shirika la kimataifa la chakula pamoja na Umoja wa mataifa kufadhili miradi ya kilimo .

    Waziri wa kilimo nchini humo Hassab Al Nabi amesema ameahidi kuongeza asilimia 50 kwenye bajeti ya maendeleo ikiwemo ajira kwa vijana na wanawake.

    Awamu ya kwanza ya mradi wa maendeleo ilioanzishwa mwaka 2015 imefanikiwa kupunguza idadi ya umaskini.

    Ripoti ya hivi majuzi ya kimataifa imeonyesha kwamba zaidi ya watu milioni 821 duniani wanaishi katika umaskini ikiwa ni asilimia 11 ya watu wote duniani .

    Eneo la chini ya jangwa la sahara pamoja na kusini mwa Asia ni miongoni mwa maeneo yalioathirika pakubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako