• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:CRDB kuimarisha sekta ya benki

    (GMT+08:00) 2018-10-22 20:19:25

    Sekta ya benki nchini Tanzania inatarajiwa kuimarika katika miaka ijayo.

    Mkurugenzi Mtendaji mpya wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela ameweka wazi mipango yake mitano ya kuinua sekta ya benki nchini ikiwemo uwekezaji katika mifumo ya kidijitali na kutumia mitandao ya kijamii kuwafikia wananchi wengi wa vijijini.

    Akizungumza jijini Dar es Salaam leo (Oktoba 10, 2018), wakati wa akitambulishwa rasmi kuiongoza benki hiyo, amesema mifumo hiyo itawezesha kuwafikia wateja wengi kwa urahisi popote walipo na kuwaondolea ulazima wa kwenda kwenye matawi ya benki hiyo yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini.

    Amebainisha kuwa kuna maeneo ambayo benki hiyo haijafika, lakini kwa kutumia simu ya mkononi mteja atapata huduma zote za kibenki popote alipo.

    Hilo litaenda sambamba na kusogeza karibu huduma za kibenki kwa wateja ikiwemo kufika katika wilaya zote ifikapo mwaka 2022 na kuongeza idadi ya mawakala wa FahariHuduma kila kona ya nchi.

    Nsekela amebainisha kuwa mkakati mwingine ni kuboresha mifumo ya utoaji wa huduma kwa wateja ili ziendane na mahitaji halisi ya wananchi na soko kwa kuimarisha mahusiano na wateja wao.

    Amefafanua kuwa chini ya uongozi wake ataimarisha uhusiano na serikali na wadau wengine ili kuongeza wigo wa biashara na uwekezaji katika sekta mbalimbali za maendeleo.

    Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo, Ally Laay emesema wataendelea kutoa ushirikiano na kuwa wameamua kumpumzisha aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk Charles Kimei kabla ya muda wake kumalizika kwababu ni vigumu kwa benki hiyo kuwa na wakurugenzi wawili kwa wakati mmoja.

    Bodi hiyo imeeleza kuwapo kwa kipindi cha mpito cha takribani miezi minane ambacho Mkurugenzi Mtendaji mpya aliyetambulishwa leo angefanya kazi na Dk. Kimei aliyemaliza muda wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako