• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China afanya tena ukaguzi mkoani Guangdong baada ya miaka sita

    (GMT+08:00) 2018-10-23 17:03:42

    Rais Xi Jinping wa China leo amewasili mjini Zhuhai, mkoani Guangdong baada ya miaka sita, na kufanya ukaguzi na uchunguzi.

    Baada ya mkutano wa 18 wa wajumbe wa Chama cha Kikomunisiti cha China CPC, rais Xi amechagua mkoa wa Guangdong kama kituo cha kwanza cha ukaguzi wa kimikoa. Rais Xi amesema, amekwenda Guangdong kwa kuwa mkoa huo unaongoza katika sera ya ufunguaji mlango na mageuzi.

    Katika ziara yake, rais Xi ametembelea eneo jipya la teknolojia ya juu la Hengqin la mji wa Zhuhai na kampuni ya vifaa vya kielektroniki ya Gree. Akiwa kwenye eneo la Hengqin, Rais Xi amesema, anafuatilia kila hatua ya maendeleo ya eneo hilo, na katika miaka kumi iliyopita, eneo hilo limepata maendeleo makubwa. Amesema inapaswa kutosahau lengo la mwanzo na kulifanya eneo hilo liwe na uhai mkubwa zaidi wa uvumbuzi na maendeleo.

    Rais Xi pia ametemebelea kampuni ya Gree na kusema, utengenezaji wa bidhaa ni umuhimu wa uchumi halisi, na kiini cha viwanda vya utengenezaji ni uvumbuzi. Amezitaka kampuni zote zifanye juhudi kuendeleza uvumbuzi na teknolojia mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako