• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziara ya waziri mkuu wa Japan nchini China yatarajiwa kuhimiza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili

    (GMT+08:00) 2018-10-23 19:13:26

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Hua Chunying leo hapa Beijing amesema, China ina imani kuwa ziara ya waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe nchini China itasaidia kuhimiza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, na kuuhimiza uhusiano kati yao upate maendeleo kwa msingi wa kurudi upya kwenye njia sahihi.

    Bi. Hua amesema, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara ni sehemu muhimu ya uhusiano kati ya China na Japan. Hivi sasa China inatekeleza hatua mpya za kufungua zaidi mlango, hii itatoa fursa kubwa zaidi na kuweka mustakabali mzuri zaidi kwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

    Bi. Hua amesema, wakati wa ziara ya Bw. Shinzo Abe hapa China, pande hizo mbili zitafanya mkutano wa kwanza kuhusu ushirikiano kwenye soko la upande wa tatu kati ya China na Japan, pia zitajadili kuimarisha ushirikiano kwenye teknolojia ya juu na mambo ya kifedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako